Mkimbizi 101

Mkimbizi 101

Kirago

“Nataka kwenda nyumbani, lakini nyumbani ni mdomo wa papa nyumbani ni pipa la bunduki na hakuna mtu ambaye angeondoka nyumbani isipokuwa amefukuzwa na nyumbani ili kuacha kile usichoweza kuaca, hata ni binadamu.”

–Warsan Shire, Poet

Watu wote wanastahili kuwa mali.

Mkimbizi ni nani?

Wakimbizi ni wanaume, wanawake na watoto wanaokimbia vita, mateso na misukosuko ya kisiasa ambao wamevuka mipaka kutafuta usalama katika nchi nyingine. Wengi hatimaye hurejea nyumbani kukiwa salama, wengine hukaa katika makazi ya muda ya wakimbizi, na sehemu ndogo huhamia katika nchi ya tatu, kama vile Malekani.

Mkimbizi ni nani?

Kama mkimbizi, mtafutaji wa nchi ya usalama pia ni mtu ambaye ameiacha nchi yake na anaogopa kurudi nyumbani kwa sababu ya woga uliojengeka wa kuteswa kutokana na rangi yake, dini, utaifa,au uanachama katika kundi fulani la kijamii au kundi la kisiasa. Tofauti na wakimbizi,wanaopokea hadhi hii ya uhamiaji kutoka kwa idara ya serikali kabla ya kuwasili kwao Marekani,watu wanaotafuta hifadhi wanaomba na wanapewa hadhi hii wakati tayarii wamefika Marekani.

Wakimbizi wanaenda wapi?

Asilimia 85 ya wakimbizi duniani waliohamishwa nje ya nchi wanahifadhiwa na nchi zenye kipato cha chini au cha kati. Uturuki imechukuwa wakimbizi milioni 3.6, zaidi ya nchi nyingine yoyote, ikifuatiwa na Columbia, Pakistan, Uganda na Ujerumani, kila moja ikiwa na zaidi ya watu milioni 1.

Nini inatokea baada ya mtu kuwa mkimbizi?

Wakimbii wengi wanaweza kurejea nyumbani baada ya mzozo au kipindi cha ukosefu wa utulivu. Baadhi ya wakimbizi, hata hivyo, wanalazimishwa kubakikatika makazi mapya ya wakimbizi ikiwa nchi yao inabakia kutokuwa na utulivu au kama wana hofu ya msingi ya kuteswa. Wakimbizi wakati mwingine wana fursa ya kujenga maisha mapya katika nchi ambako wanatafuta hifadhi. Asilimia ndogo sana ya wakimbizi duniani wamepewa makazi mapya katika nchi ya tatu, kama Marekani. Uhamisho wa Marekani unaweza kuwa mchakato wa polepole; wakimbizi wengi hukaa hadi miaka 20 wakisubiri kuhamishwa.

Nani hulipa mkimbizi kusafiri?

Wakimbizi lazma walipe mikopo yote ya usafiri mara tu baada ya kuwasili Marekani.

Je, wakimbizi huchagua jiji lao la makazi mapya?

Wakimbizi hawachagui mji wao wa makazi mapya. Isipokuwa kama kuna mwanafamilia wanaoungana naye, wakimbizi wako chini ya mchakato wa kuwapa makazi mapya katika ngazi ya kitaifa na wanakuwa na chaguo dogo pale ambapo wana makazi mapya.

Je, wakimbizi wanaruhusiwa kisheria kuwa Marekani?

Wakimbizi wanaokuja Marekani hupitia mchakato mrefu wa kukaguliwa na kusubiri. Wanaalikwa na Idara ya Jimbo na ni wakaazi halali kwenye njia kuu ya uraia. Ni lazima wasubiri mwaka mmoja kupata kadi ya kijani na miaka mitano kutuma maombi ya uraia.

Kwa nini Karibu?

Nipe uchovu wako, masikini wako, Umati wako uliosongamana wanaotamani kupumua bure, Takataka mbaya ya ufuo wako uliojaa. Nipelekeeni hawa, wasio na makazi, wenye tufani, nainua taa yangu kando ya mlango wa dhahabu.

– Emma Lazaro Novemba 2, 1883 (Maneno yaliyochapishwa kwenye Sanamu ya Uhuru)

Makazi mapya nchini Marekani na Michigan

Tangu 1975, Marekani imepokea zaidi ya wakimbizi milioni tatu kutoka duniani kote, na wakimbizi hawa wamejenga maisha mapya kwa familia zao katika majimbo yote 50. Lansing imekuwa sehemu ya safari hii ya kukaribisha tangu mwanzo na imewapa makazi mapya takriban wakimbizi 20,000 katika kipindi cha miongo minne na nusu iliyopita. Tunapokaribisha wakimbizi, wanabadilisha maisha yetu na jamii kuwa bora.

Marekani inawapa makazi wakimbizi walio hatarini zaidi na imekuwa kiongozi wa makazi mapya duniani kwa miongo kadhaa.

Wakimbizi na familia zao wamejiingiza katika mfumo wa jamii ya Marekani. Ni majirani zetu, marafiki zetu na wenzetu. Wao ni walimu, wamiliki wa biashara na wanachangia vyema kwa jamii kote nchini.

Wakimbizi wana jukumu muhimu katika ukuaji wa Michigan–kiuchumi, kijamii na kitamaduni–kusaidia kufanya jimbo letu kuwa na nguvu na ustawi. Wakimbizi Wapya ni wamiliki wa biashara, wamiliki wa nyumba, walipa kodi, wanafunzi, walimu na majirani. Tunayo heshima kubwa kuunga mkono majirani wetu wapya wanapokita mizizi na kujihisi kuwa washiriki katika jamii.